Makka
Sura Al-Alaq

Aya

19

Mahali iliteremshwa

Makka

SURAT AL-A'LAQ 

(Imeteremka Makka)

Katika Sura hii upo wito wa kusoma na kujifunza, na kwamba aliye weza kumuumba mtu kutokana na asli nyonge ni Mweza wa kumfunza kuandika kwa kudhibitia ilimu  na kutimizia kufahamu, na amfunze aliyo kuwa hayajui. Kwani Yeye Subhanahu ndiye Mwenye kummiminia ilimu mwanaadamu. Na Sura inanabihisha kwamba utsjiri na nguvu huenda zikampelekea mtu kupindukia mipaka ya Mwenyezi Mungu, lakini marejeo ya wote ni kwa Mwenyezi Mungu mwishoni. Na mazungumzo yanamwelekea kila mwenye kusilihi kusemezwa kuwaonya hao majeuri wanao pinga kheri, kuwaonya kuwa watakuja kushikwa kwa nywele zao za utosi wakibururwa Motoni; hawatofaliwa na wasaidizi wowote. Na Sura inakhitimisha kwa kuwataka wende kinyume na hao wenye inda wanao kadhibisha, na wajijongeze kwa utiifu kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.