Basi aliposikia yule bibi masengenyo yao, aliwaita, na akawawekea matakia ya kuegemea, na akampa kila mmoja wao kisu. Akamwambia Yusuf: "Jitokeze mbele yao." Basi walipomwona, waliona ni kitu kikubwa kabisa, na wakajikatakata mikono yao. Wakasema: Hasha Lillahi (Ametakasika Mwenyezi Mungu)! Huyu si mwanadamu. Huyu si isipokuwa Malaika mtukufu.