Makka
Sura Al-Muddaththir

Aya

56

Mahali iliteremshwa

Makka

SURAT AL-MUDDATHTHIR 

(Imeteremka Makka) 

Sura hi tukufu inamhimiza Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w. awaonye watu wake, na amtukuze Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ayaache yasiyo faa kutokana naye, na imesimulia khabari za kupulizwa barugumu na shida za adhabu zitazo washukia makafiri. Na inamuamrisha Mtume s.a.w. amwachilie mbali anaye pinga fadhila alizo fanyiwa na kisha anatumai bado azidishiwe bila ya kutambua wala shukrani. Na Sura imebainisha ipi kulikuwa kufikiri kwa huyo mwenye kupinga na kuikataa Qur'ani, na ikafafanua vipi itakuwa adhabu yake katika Moto wa Saqar ambao unaelezwa kwa njia vya kutisha na kukhofisha. Na ikataja khabari za nafsi kwa zinavyo chuma kheri au shari, na ikaeleza hali ya watu wa mkono wa kulia na wanavyo wakejeli wakosefu kwa kuwauliza nini kilicho wasukumiza Motoni. Na Sura imekhitimisha kwa kusimulia kuwa Qur'ani ni ya mwenye kutaka kuwaidhika, na wenye kuwaidhika ndio watu wachamngu na ndio wenye kupata msamaha.