Aya
42
Mahali iliteremshwa
Makka
SURAT A'BASA
(Imeteremka Makka)
Sura hii imeanza kwa kumlaumu Nabii Muhammad s.a.w. kwa kumpuuza Ibnu Maktoum alipo mjia kutafuta ilimu na uwongofu. Naye Nabii s.a.w. alikuwa kashughulika kuwalingania Dini baadhi ya mabwana wa Kikureshi kwa kutaraji ili watamwitikia, ili kwa kusilimu kwao wange silimu watu wengi. Kisha inamkumbusha binaadamu kwa neema alizo pewa na Mwenyezi Mungu kuumbwa kwake mpaka kufufuliwa kwake. Na ikakhitimisha kwa kusimulia za Siku ya Kiyama, ikibainisha kwamba watu siku hiyo ni makundi mawili, kundi la Waumini lenye furaha, na kundi la makafiri wapotovu.