Aya:
4
Mahali iliteremshwa:
Makka
SURAT AL-IKHLAS'
(Imeteremka Makka)
Nabii s.a.w. aliulizwa khabari za Mola wake Mlezi, akaamrishwa katika Sura hii ajibu kwamba Yeye ni Mwenye kukusanya sifa zote za ukamilifu, ni Mmoja, wa Pekee Mwenye kukusudiwa daima katika haja, Mwenye kujitosha hamhitajii yeyote nwenginewe, ametakasika na kuwa na mfano, hakuzaa wala hakuzaliwa, wala hana mwenzie katika viumbe vyake.