Aya:
44
Mahali iliteremshwa:
Makka
SURAT AL-MAA'RIJ
(Imeteremka Makka)
Katika Sura hii tukufu kipo kitisho kwa Siku ya Kiyama, na kutia khofu kwa urefu wake, na vitisho vikubwa vikubwa, na adhabu ambazo hazikubali wi kutolewa fidia hata ya wana, wala mke, wala ndugu, wala ukoo mzima. Bali haikubaliwi fidia ya watu wa dunia nzima.
Na katika Sura hii unatolewa kombo udhaifu wa binaadamu wakati wa shida na neema, isipo kuwa aliye okolewa na Mwenyezi Mungu kwa uchamngu, na vitendo vyema. Hao wanasalimika na udhaifu huo.
Humo vile vile yanaelezwa kuchukiza tabia ya makafiri ya kuwa na tamaa ya uharibifu. Na mwishoni anausiwa Mtumewa Mwenyezi Mungu s.a.w. awawachilie mbali na upumbavu wao na mchezo wao mpaka wakutane na siku yao waliyo ahidiwa.