Aya
30
Mahali iliteremshwa
Makka
SURAT AL-MULK
(Imeteremka Makka)
Sura hii inaitwa Surat Al-Mulk kwa kutokana na neno Al-Mulk, yaani Ufalme, linalo tokea katika Aya ya kwanza katika Sura. Na muhimu ya makusudio ya Sura hii tukufu ni kuelekeza fikra na nadhari zizingatie athari ya uweza wa Mwenyezi Mungu ulio zagaa katika nafsi za watu na katika viumbe vya Mwenyezi Mungu mnavyo viona katika ardhi na mbinguni upeo wa macho yenu, ili hayo yawe ndiyo njia ya kupelekea kumuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.
Na pia Sura hii inabainisha hali ya makafiri ambao watatupwa katika Jahannamu, na watasikilizana mikoromo yao, na wataungua katika Moto wake, na wataungama madhambi yao, na watajuta kwa watavyo ishia, watapo wauliza Malaika kwa kuto mwitikia Mtume alipo waita na akawahadharisha.
Na ama walio mkhofu Mola wao Mlezi, na wakamuamini, hao watapata maghfira na msamaha kwa makosa yaliyo waporonyoka, na ujira mkubwa kwa mema waliyo yatanguliza na wakayatenda.