Ingia
🚀 Jiunge na Changamoto yetu ya Ramadhani!
Jifunze zaidi
🚀 Jiunge na Changamoto yetu ya Ramadhani!
Jifunze zaidi
Ingia
Ingia
Taarifa ya Sura
011

Sura Hud

Aya:

123

Mahali iliteremshwa:

Makka

Ali Muhsin Al-Barwani - Swahili Translation of Al-Muntakhab

SURAT HUD 

(Imeteremka Makka)

Surat Hud ni Sura ya Makka. Ina Aya 123. Imeanza kwa kuisifu Qur'ani Tukufu, na kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na kuonya, na kubashiria. Kisha ikabainisha uwezo wa Mwenyezi Mungu na kuwa Yeye ndiye Mola Mlezi. Na ikaeleza hali za watu katika kuzipokea kwao neema zake Mola Mlezi, na adhabu zake. Kisha ikataja cheo cha Qur'ani, na kufuru za makafiri bila ya udhuru wowote kwa ukafiri wao, na malipo ya Waumini.

Naye Subhanahu baada ya hayo amesimulia hadithi za Manabii, na majadiliano ya kaumu zao nao, na kuwateremkia makafiri adhabu ya duniani na kuokoka kwa Waumini. Subhanahu wa Taa'la akataja hadithi ya Nuhu kwa kupambanua zaidi kuliko ilivvo kuwa katika Surat Yunus. Humu imeelezwa fikra za kafiri na inadi yake, na imebainishwa ilivyo mteremkia chuki. Na baada ya hadithi ya Nuhu Mwenyezi Mungu Subhanahu ametaja kisa cha A'ad pamoja na Nabii wa Mwenyezi Mungu Hud, kwa kueleza wazi mawazo ya ukafiri, na yaliyo wateremkia makafiri juu ya kuwa walikuwa na nguvu na wakali.

Kisha kikatajwa mfano wa hayo kisa cha Nabii wa Mwenyezi Mungu, Saleh pamoja na kabila la Thamud, na tena kisa cha Nabiyyu Llah na rafiki yake, Ibrahim. Kisha hadithi wa Nabiyyu Llah, Lut. Kisha kisa cha Nabiyyu Llah, Shua'ib. 

Kisha Subhanahu wa Taala ametaja nini mafunzo ya hadithi hizi za kweli, na akamalizia Subhanahu kwa kuwataka Waumini watende mema, na wangojee malipo. Tena ukatajwa ujuzi ulio kamilika wa Mwenyezi Mungu Aliye takasika na kutukuka na waajibu wa kumtegemea Yeye.

He has revealed to you ˹O Prophet˺ the Book in truth, confirming what came before it, as He revealed the Torah and the Gospel
— Dr. Mustafa Khattab, the Clear Quran
Notes placeholders
Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu

Ayatul Kursi

Yaseen

Al Mulk

Ar-Rahman

Al Waqi'ah

Al Kahf

Al Muzzammil

Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa