Makka
Sura Al-Buruj

Aya

22

Mahali iliteremshwa

Makka

SURAT AL-BURUUJ 

(Imeteremka Makka)

Sura hii ni ya maliwaza na kuwapa mawaidha Waumini, na kuwatisha na kuwaonya wenye inadi. Imeanzia kwa kiapo chake Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa madhaahiri yanayo onekana ya uweza wake ya kwamba wapinzani wanao waudhi Waumini watafukuzwa kwenye uwanja wa rehema, kama walivyo fukuzwa walio kwenda mwendo wao katika mataifa yaliyo tangulia. Na Sura ikaingia kusimulia kisa cha hao majabari walivyo watendea Waumini, na ikafuatiza kwa kuwapa ahadi Waumini na kuwakhofisha majeuri, na kwamba Haki katika kila zama hupingwa na wapinzani. Na kwamba Qur'ani, ambayo ndiyo mwega wa Haki, na wangaikadhibisha watu fulani, lakini hiyo iko mbali kabisa na shaka, kwa sababu hakika hiyo iko katika Lauh'un Mahfuudh, Ubao Ulio Hifadhiwa ulioko kwa Mwenyezi Mungu.