Aya:
21
Mahali iliteremshwa:
Makka
Ali Muhsin Al-Barwani - Swahili Translation of Al-Muntakhab
SURAT AL-LAYL
(Imeteremka Makka)
Mwenyezi Mungu Mtukufu ameapa kwa viapo vitatu juu ya kuwa vitendo vya watu vinakhitalifiana, baadhi yake ni vya uwongofu, na baadhi yake ni vya upotofu. Mwenye kutoa, na akamchamngu, na akawafiki tabia yenye kukusanya kheri, basi Mwenyezi Mungu atamsahilishia mambo yake kwa wepesi. Na mwenye kufanya ubakhili, na akajiona hana haja na mtu, na akakanusha tabia zenye kukusanya Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi kuingia mashakani. Na wala mali yake hayatamfaa kitu kumwokoa akitumbukia katika adhabu! Na Aya zikabainisha baada ya hayo kwamba hakika Mwenyezi Mungu amechukua jukumu kubainisha njia za uwongofu kwa fadhila zake, na kwake yapo mambo ya maisha mawili, ya Akhera na ya duniani. Na kwamba hakika Yeye amekwisha onya kwamba Moto watauingia waovu na watauepuka walio wema.