Aya:
286
Mahali iliteremshwa:
Madina
Ali Muhsin Al-Barwani - Swahili Translation of Al-Muntakhab
SURA AL- BAQARA
(Imeteremka Madina)
Sura hii imeteremka Madina baada ya Hijra. Nayo ndiyo sura ndefu kuliko zote katika Qur'ani Tukufu kwa mujibu wa mtungo wa Msahafu. Sura hii imeanzia kueleza kwa tafsili yale yaliyo malizikia Sura ya Al Faatiha. Imetaja kuwa Qur'ani ndiyo msingi wa uwongofu, na imewataja wale walio neemeshwa na Mwenyezi Mungu kwa kupata radhi zake, na wale walio kasirikiwa, nao ni makafiri na wanaafiki.
Sura imeeleza ukweli wa Qur'ani, na kwamba wito wake ni wa kweli usio na shaka. Kisha ikaingia kueleza namna tatu za watu: Waumini, Makafiri na Wanaafiki. Na ikataja Daa'wa, Mlingano au Wito, kuwaita watu wamuabudu Mwenyezi Mungu pekee, na ikawaonya makafiri, na ikawapa bishara njema Waumini. Baadaye ikawaelekea Wana wa Israili khasa kwa kuwaita na kuwakumbusha siku za Mwenyezi Mungu, na kwa vituko vyao na Musa (AS) na kuwakumbusha khabari za Ibrahim na Ismail na walivyo ijenga Al Kaaba. Hayo yamechukua karibu nusu ya Sura. Mazungumzo yakawageukia Waumini wazingatie yaliyo wapata Mayahudi na Wakristo.
Mazungumzo yakaingia kuwasemeza watu wa Qur'ani kwa kuwakumbusha mamba ambayo umma wa Musa na umma wa Muhammad walivyo shirikiana katika kutukuzwa Ibrahim na kuongoka kwake na nasaba yake, na kwa kutaja kibla na mfano wa hayo.
Kisha yakaja mazungumzo juu ya Tawhid (Upweke wa Mwenyezi Mungu) na kukumbusha Ishara za Mwenyezi Mungu zenye kumuashiria Yeye. Na yakaja masimulizi juu ya ushirikina, na juu ya vyakula vilivyo harimishwa, na kwamba kuharimisha na kuhalalisha ni haki ya Mwenyezi Mungu pekee yake.
Sura ikaingia kubainisha misingi ya wema, na kutaja baadhi ya hukumu za Saumu, na wasia, na kula mali ya watu kwa dhulma, na kisasi, na vita, na Hija, na ulevi, na kamari. na ndoa na talaka, na kunyonyesha, na eda na mengineyo. Hali kadhaalika yamezungumzwa mambo ya itikadi kwa jumla kama Utume, Tawhidi, kufufuliwa. Yametajwa mas-ala ya kutoa sadaka na Zaka, riba, biashara, kuandikiana madeni Mwishoe Sura yakhitimisha kwa dua ya Waumini kumwomba Mola wao Mlezi awanusuru na awasaidie.
Sura hii imekusanya misingi kadhaa wa kadhaa. Miongoni mwayo ni: