Aya
35
Mahali iliteremshwa
Makka
SURAT AL AH'QAAF
(Imeteremka Makka)
Sura hii tukufu inasimulia kuteremka kwa Qur'ani kutokana na Mwenyezi Mungu, na kupasa kuiamini na kumuamini Muhammad s.a.w. na kuisadiki Siku ya Kiyama. Na imekusudia kunabihisha watu wazingatie yaliyo wapata walio tangulia walio muasi Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na imeita watu washughulikie kuwafanyia wema wazazi wawili,. na kuzitunza haki zao.
Na hii Sura imeelezea kisa cha baadhi ya majini waliyo isikia Qur'ani tukufu, wakaambizana waisikilize. Wakaiona kuwa inathibitisha yale yale waliyo kuja nayo Mitume wa kabla ya Muhammad s.a. w., inaongoa kwendea Haki na kwenye Njia Iliyo Nyooka. Wakaiamini; na wakawataka wenzao wafuate yale yale. Ikamalizikia hadithi kwa wito wa kumtaka Nabii s.a.w. avumilie vile anavyo kadhibishwa na kaumu yake, na kumliwaza katika hayo kwa waliyo yastahamilia Mitume wa kabla yake wenye azma ngumu.