Aya
19
Mahali iliteremshwa
Makka
SURAT AL-INFIT'AAR
(Imeteremka Makka)
Sura hii imeeleza baadhi ya vitisho vya Saa ya Kiyama kwa njia ya kutangaza kuwa
hakika litatokea jambo katika siku ambayo kila mtu atajua nini alilo litanguliza na nini alilo liakhirisha. Tena Aya zikaingia kumhadharisha mwanaadamu aliye danganyika na Mola wake Mlezi aliye muumba akamweka sawa, akamjenga kwa namna ya pekee, na kwa umbo bora kabisa. Inathibitisha Sura kuwa huyo mtu anaikadhibisha Siku ya Malipo, na inatilia mkazo kuwepo Malaika juu yake, walinzi mahashumu, waandishi. Na ikamalizia kusema kuwa watu wema watapata neema. Na wapotovu hawatapata ila Jahannamu, watakayo iingia Siku ya Kiyama, siku ambayo nafsi haitoweza kuimilikia nafsi nyengine chochote. Na amri yote itakuwa ni ya Mwenyezi Mungu tu.