Aya
3
Mahali iliteremshwa
Madina
SURAT ANNAS'R
(Imeteremka Madina)
Sura hii imemtaka Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w ukija msaada wa Mwenyezi Mungu na ushindi, na akaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi kwa kutua mambo yake na kutukuka neno lake na kumkamilishia Mwenyezi Mungu basi amtakase Mola wake Mlezi kwa kumsifu, na amtakase na kila lisio mwelekea, na amwombe msamaha kwa nafsi yake na kwa Waumini, kwa sababu hakika Yeye ni Mwingi wa kukubali toba za waja wake, na anasamehe makosa.