Ingia
🚀 Jiunge na Changamoto yetu ya Ramadhani!
Jifunze zaidi
🚀 Jiunge na Changamoto yetu ya Ramadhani!
Jifunze zaidi
Ingia
Ingia
Taarifa ya Sura
021

Sura Al-Anbiyaa

Aya:

112

Mahali iliteremshwa:

Makka

Ali Muhsin Al-Barwani - Swahili Translation of Al-Muntakhab

SURATUL ANBIYAA 

(Imeteremka Makka)

HII NI SURA iliyo teremka Makka baada ya Surat Ibrahim. Aya zake ni 112 Inabainisha kukaribia Kiyama na hali washirikina wameghafilika nacho. Nao walidai kuwa Mtume hatokuwa binaadamu, na pengine wakisema kuwa hii Qur'ani ni uchawi na pengine kuwa ni mashairi, na pengine ni ndoto za ovyo ovyo. Na maonyo yapo mbele yao. Na Mitume wote hawakuwa ila ni wanaadamu tu kama Muhammad s.a.w., na walio watangulia kabla yao walisema uwongo kama walivyo sema uwongo Makureshi. 

Mwenyezi Mungu aliwajaalia ajali yao, kwani Yeye ni Mweza wa kuteketeza na kubakisha, na ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na ardhi. Na Malaika kila walipo wanamtakasa kwa kumsabihi Mwenyezi Mungu Mtukufu wala hawasiti. Na hakika kwenda sawa mbingu na ardhi ni dalili kuwa Muumba wake ni Mmoja, kwani lau kuwa wangeli shirikiana waumbaji mambo yangeli fisidika. Ne Mitume wote wamekuja na amri ya kuabudiwa Mwenyezi Mungu peke yake. Wala hana mwana, wala asiseme yeyote kuwa yeye ni mungu pamoja na Mwenyezi Mungu. Wasemao hivyo malipo yao ni Jahannamu. 

Na Subhanahu kabainisha utukufu wa viumbe vyake, na ajabu za uumbaji wake wa mbingu na ardhi. Na akabainisha hali ya washirikina na makafiri. Naye Subhanahu wa Taa'la amenabihisha vipi Mwenyezi Mungu Mtukufu anavyo wahifadhi watu, na akaashiria Subhanahu nini malipo ya makafiri Siku ya Kiyama, Na akataja hadithi ya Musa na Harun pamoja na Firauni, na hadithi ya Ibrahim pamoja na kaumu yake, na alivyo mneemesha kwa dhuriya wema Naye Subhanahu wa Taa'la ametaja hadithi ya Luut na kaumu yake, na walivyo angamizwa, na hadithi ya Nuhu (AS) na ukafiri wa kaumu yake, na walivyo teketezwa isipo kuwa walio amini. 

Kisha Subhanahu wa Taa'la akaashiria hadithi za Sulaiman, na Daud, na Ayub, na Ismail, na Idris, na Dhulkifli, na Dhunnuun, na Maryamu. Na akataja khabari za Juj na Maajuj. Naye Subhanahu amebainisha vitendo vyema na matunda yake, na malipo watakayo lipwa wenye kumchamngu na wakatenda mema, na hali yao Siku ya Kiyama, na rehema ya Mwenyezi Mungu katika Ujumbe wa Muhammad, na maonyo ya Mwenyezi Mungu kwa washirikina. Na kwamba hakika amri yote ni yake Yeye anavyo hukumu, na Yeye ndiye Mbora wa mahakimu.

He has revealed to you ËąO ProphetËş the Book in truth, confirming what came before it, as He revealed the Torah and the Gospel
— Dr. Mustafa Khattab, the Clear Quran
Notes placeholders
Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu

Ayatul Kursi

Yaseen

Al Mulk

Ar-Rahman

Al Waqi'ah

Al Kahf

Al Muzzammil

Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa