Aya
28
Mahali iliteremshwa
Makka
SURAT NUH'
(Imeteremka Makka)
Sura hii tukufu imefafanua kisa cha Nuh'u a.s. pamoja na kaumu yake. Ikasimulia khabari za wito wake kwa dhaahiri. kisha kwa siri na kwa dhaahiri. Na ikaeleza mashtaka yake kumshtakia Mwenyezi Mungu juu ya walivyo mpuuza, na inda walio mfanyia, na ikasajili kukakamia kwao kuyaabudu masanamu mpaka wakastahiki kupata adhabu ya Mwenyezi Mungu. Nuh'u alipo kata tamaa nao kuukubali wito wake, aliwaapiza wahiliki na waangamie, na akajiombea nafsi yake, na wanawe, Waumini wanaume, na Waumini wanawake, wapate msamaha.