Ingia
🚀 Jiunge na Changamoto yetu ya Ramadhani!
Jifunze zaidi
🚀 Jiunge na Changamoto yetu ya Ramadhani!
Jifunze zaidi
Ingia
Ingia
Taarifa ya Sura
019

Sura Maryam

Aya:

98

Mahali iliteremshwa:

Makka

Ali Muhsin Al-Barwani - Swahili Translation of Al-Muntakhab

SURAT MARYAM  

(Imeteremka Makka) 

Hii ni Sura iliyo teremka Makka, na hamna Aya za Madina ila Aya 57 na 71. Hisabu ya Aya zake ni 98. Imeanzia kwa harufi moja moja kama Sura nyingi nyenginezo. Ndani ya Sura hii kipo kisa cha kuzaliwa Yahya bin Zakariya (Alayhima Ssalam). Zakariya alitamani mwana na hali kesha fikilia ukongwe na mkewe ni tasa. Na kimetajwa pia kisa cha Bibi Bikra Maryam ((AS)) na kumzaa kwake Masihi ((AS)). Kisha kikatajwa kisa cha Ibrahim (A.S) na Wito wake kulingania Upweke Mwenyezi Mungu, na alivyo mtaka babaake aache kuabudu masanamu, na majibizano wa yao yaliyo jiri kwa ajili ya masanamu, na madaraka ya Shetani. 

Pia wameashiriwa Manabii wengine katika dhuriya za Ibrahim, nao ni Ismail na Is-haq na dhuriya wa Is-haq. Tena kikagusiwa kisa cha Idris ((AS)). Na tena Mwenyezi Mungu Subhanahu akataja khabari za walio fuatia wakaja baada ya Manabii, watu watiifu na wengine maasi. Na akataja kuwa Pepo ndiyo malipo ya Waumini, na Moto ni malipo ya makafiri, na akazitaja hali za makafiri katika Jahannamu. Na tena Subhanahu akagusia ya wapotovu wanao sema kwamba Mwenyezi Mungu ana mwana.

Na Subhanahu amebainisha cheo cha Qur'ani, na amewaonya makafiri, na amepiga mifano ya watakavyo teketea wanao waasi Manabii. Na akaashiria kwamba hao wamepotea kabisa, hawakuacha hata ukumbusho.

He has revealed to you ËąO ProphetËş the Book in truth, confirming what came before it, as He revealed the Torah and the Gospel
— Dr. Mustafa Khattab, the Clear Quran
Notes placeholders
Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu

Ayatul Kursi

Yaseen

Al Mulk

Ar-Rahman

Al Waqi'ah

Al Kahf

Al Muzzammil

Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa