Sura Al-Mursalat

Aya

50

Mahali iliteremshwa

Makka

SURAT AL-MURSALAAT 

(Imeteremka Makka)

Lilio muhimu kabisa katika yaliyo kusanywa na Sura hii tukufu ni maneno yaliyo khusu kufufuliwa, na Kiyama, na dalili za kuthibitisha kuwa kitatokea, na kutishwa  kwa waliyo yakataa hayo, na kurudishwa kutishwa huko kwa "Ole wao" mara kumi, na kuwatisha kwa unyonge na adhabu itayo wapata; na kubashiriwa wachamngu kwa starehe na neema watazo zikuta, na mwisho wake masaibu yatayo wapata makafiri wasio iamini Qur'ani.