Ingia
🚀 Jiunge na Changamoto yetu ya Ramadhani!
Jifunze zaidi
🚀 Jiunge na Changamoto yetu ya Ramadhani!
Jifunze zaidi
Ingia
Ingia
Taarifa ya Sura
031

Sura Luqman

Aya:

34

Mahali iliteremshwa:

Makka

Ali Muhsin Al-Barwani - Swahili Translation of Al-Muntakhab

SURAT LUQMAN 

(Imeteremka Makka)

Imeanza Sura hii tukufu kwa kueleza khabari za hichi Kitabu na uwongofu na rehema ziliomo ndani yake. Na wamesifĩwa watu wema kwa kuwa wana utiifu kwa Mwenyezi na wanaiamini Akhera, na watapata mafanikio. Na kinyume cha hayo yametajwa ya walio potea, wenye kiburi. Na wamebashiriwa Waumini kuwa watapata malipo mazuri katika makaazi ya Peponi. Na macho yanatakiwa yaangalie Ishara za ulimwengu zinazo onyesha uweza wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Upweke wake. Na Sura hii inawakabili makafiri kwa kuwaambia kwamba kwa hakika Mwenyezi Mungu wanaye muwekea washirika ameumba asicho kiweza yeyote asiye kuwa Yeye kukiumba. Tena Sura ikaingia kutaja wasia wa Luqman kumuusia mwanawe mausio yaliyo changanyika na mausio ya mtu na wazazi wake. Na ikaeleza mambo aliyo yatiisha Mwenyezi Mungu kwa faida ya mwanaadamu, na neema zinazo onekana na zisio onekana alizo mjazia mwanaadamu.

Na ikaeleza khabari za wanao jadili mambo yaliyo mkhusu Mwenyezi Mungu bila ya ujuzi, na wanao toa udhuru kwa upotovu wao kuwa wanawafuata waliyo kuwa wakiyafuata baba zao. Na Sura ikamsifu anaye uelekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu naye akawa ni mtenda mema, na ikamnasihi Mtume asihuzunike kwa kukataa kwa mwenye kukufuru, kwani marejeo ya huyo ni kwa Mwenyezi Mungu. Na ikafafanua kwa wingi mambo yanayo onyesha uweza, na utukufu, na rehema.

Na Sura imeamrisha kumcha Mwenyezi Mungu, na kuogopa hisabu na malipo. Na imehadharisha ghururi, kudanganyika, na kumtii Shetani. Na ikakhitimisha kwa na kutaja kuwa Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye ujuzi kamili wa kila kitu. Na muhimu ya iliyo kusanya Sura hii ni mambo matatu: 

  • Kwanza: Kuwabashiria watu wema kuwa watapata neema na furaha, na kuwaonya makafiri kuwa watapata adhabu. 
  • Pili: Kueleza Ishara za ulimwengu na mambo yaliyo wazi yenye kuonyesha uweza wa Mwenyezi Mungu, na Upweke wake, na upeo wa utukufu wake na rehema yake. 
  • Tatu: Wasia mkuu ulio kusudiwa usalama wa itikadi, na kulinda utiifu na tabia njema.
He has revealed to you ˹O Prophet˺ the Book in truth, confirming what came before it, as He revealed the Torah and the Gospel
— Dr. Mustafa Khattab, the Clear Quran
Notes placeholders
Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu

Ayatul Kursi

Yaseen

Al Mulk

Ar-Rahman

Al Waqi'ah

Al Kahf

Al Muzzammil

Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa