Makka
Sura At-Takwyr

Aya

29

Mahali iliteremshwa

Makka

SURAT ATTAKWIR

(Imeteremka Makka)

Katika Sura hii yanaelezwa yatakayo tokea wakati wa Saa ya Kiyama na baada yake, na yanaelezwa ya kuonyesha dalili za uweza wa Mwenyezi Mungu, na kutilia mkazo cheo cha Qurani tukufu, na kupinga madai ya uzushi katika Qur'ani, na kumtakasa Mtume s.a.w. na tuhuma za wazimu, na kuwatisha na kuwaonya hao wanao endelea na upotovu, na inataka yaangaliwe mazingatio yaliyomo katika Qur’ani ambayo yatawafaa watu wenye kusimama msimamo wa sawa, na inarudisha mambo yote ya watu kwenye mapenzi ya Mola Mlezi wa walimwengu wote.