Aya
34
Mahali iliteremshwa
Makka
SURAT LUQMAN
(Imeteremka Makka)
Imeanza Sura hii tukufu kwa kueleza khabari za hichi Kitabu na uwongofu na rehema ziliomo ndani yake. Na wamesifĩwa watu wema kwa kuwa wana utiifu kwa Mwenyezi na wanaiamini Akhera, na watapata mafanikio. Na kinyume cha hayo yametajwa ya walio potea, wenye kiburi. Na wamebashiriwa Waumini kuwa watapata malipo mazuri katika makaazi ya Peponi. Na macho yanatakiwa yaangalie Ishara za ulimwengu zinazo onyesha uweza wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Upweke wake. Na Sura hii inawakabili makafiri kwa kuwaambia kwamba kwa hakika Mwenyezi Mungu wanaye muwekea washirika ameumba asicho kiweza yeyote asiye kuwa Yeye kukiumba. Tena Sura ikaingia kutaja wasia wa Luqman kumuusia mwanawe mausio yaliyo changanyika na mausio ya mtu na wazazi wake. Na ikaeleza mambo aliyo yatiisha Mwenyezi Mungu kwa faida ya mwanaadamu, na neema zinazo onekana na zisio onekana alizo mjazia mwanaadamu.
Na ikaeleza khabari za wanao jadili mambo yaliyo mkhusu Mwenyezi Mungu bila ya ujuzi, na wanao toa udhuru kwa upotovu wao kuwa wanawafuata waliyo kuwa wakiyafuata baba zao. Na Sura ikamsifu anaye uelekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu naye akawa ni mtenda mema, na ikamnasihi Mtume asihuzunike kwa kukataa kwa mwenye kukufuru, kwani marejeo ya huyo ni kwa Mwenyezi Mungu. Na ikafafanua kwa wingi mambo yanayo onyesha uweza, na utukufu, na rehema.
Na Sura imeamrisha kumcha Mwenyezi Mungu, na kuogopa hisabu na malipo. Na imehadharisha ghururi, kudanganyika, na kumtii Shetani. Na ikakhitimisha kwa na kutaja kuwa Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye ujuzi kamili wa kila kitu. Na muhimu ya iliyo kusanya Sura hii ni mambo matatu: