Ingia
🚀 Jiunge na Changamoto yetu ya Ramadhani!
Jifunze zaidi
🚀 Jiunge na Changamoto yetu ya Ramadhani!
Jifunze zaidi
Ingia
Ingia
Taarifa ya Sura
037

Sura As-Saaffat

Aya:

182

Mahali iliteremshwa:

Makka

Ali Muhsin Al-Barwani - Swahili Translation of Al-Muntakhab

SURAT ASS'AFFAT 

(Imeteremka Makka)

Sura hii imeanza kwa kiapo kwa mataifa miongoni mwa viumbe vya Mwenyezi Mungu ambayo yana sifa ya kujipanga kwa safu, na kuzuia, na kusoma. Kiapo hicho ni kuwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mmoja. Na Ishara zinashuhudia kwa hayo. Kwani Yeye ni Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, na Yeye ni Mola Mlezi wa mashariki na magharibi, ambaye aliye ipamba mbingu ya dunia kwa nyota, na akaifanya ihifadhike na muasi aliye acha utiifu wa Mwenyezi Mungu. 

Na baada ya wa kuthibitisha itikadi ya Tawhidi, Sura imeendelea kuthibitisha itikadi ya kufufuliwa. Na ikawahadharisha wenye kutia shaka kuwa huko kufufuliwa kutawazukia ghafla nao wanaona. Na ikazileta dalili za kumkinika huko, bali wepesi wa kutokea kwake, na hali wao wanayaona hayo na wanasema: Hii ndiyo Siku ya Hisabu! Na wataambiwa: Hii ndiyo Siku ya mpambanuo mlio kuwa mkiikanusha. Na watakusanywa madhaalimu na walivyo kuwa wakiviabudu. Na watasailiwa na watahojiwa. Na watakuwa wakisingiziana wao kwa wao madhambi walio yapata, na hali wote watakuwa wanashirikiana pamoja katika adhabu. Kwani walijivuna wakakataa kumuamini Mwenyezi Mungu Mmoja, na wakamsingizia Mtume wao kuwa ana kichaa na wazimu; na hali kuwa hapana shaka kuwa kawajia na Haki. Na Mitume wamesema kweli katika waliyo kuja nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na Waumini wenye ikhlasi watastareheshwa kwa kila namna ya neema. Na watazikumbuka neema za Mwenyezi Mungu: Watawatokea watu waovu, na watawaona katikati ya Moto wa Jahim. Watamhimidi Mwenyezi Mungu kwa alivyo walinda, na walivyo okoka wasifuate wito wa wale waovu. 

Baada ya hayo Sura ikaingia ikieleza mashukio ya walio dhulumu na mashukio ya Waumini. Tena ikafuatiliza kwa kueleza khabari ze Mitume wengine ili kumpoza Mtume wa Mwenyezi Mungu. na kuwapa mawaidha watu wake wanao pinga. Na baada ya hadithi mbali mbali za zama mbali mbali n watu mbali mbali, zilizo eleza cheo cha Ujumbe na Wajumbe wenyewe, Sure imetengua madai ya washirikina kwamba Mwenyezi Mungu ana mabinti na wao wana watoto wanaume. Na kwamba Yeye amewafanya Malaika ni wanawake. Na kwamba ipo nasaba ya kukhusiana baina yake na majini. Mwenyezi Mungu Ametakasika na hayo wanayo yazua. Na waja wake ndio watanusuriwa, na jeshi lake ndilo litakalo shinda. Na adhabu yake itaifanya ovu asubuhi ya wanao onywa. Na Sura ikakhitimisha wa kumtakasa Mola Mlezi wa Utukufu na hayo wanayo mzulia, Na amani ishuke kwa Mitume wote, na Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.

He has revealed to you ˹O Prophet˺ the Book in truth, confirming what came before it, as He revealed the Torah and the Gospel
— Dr. Mustafa Khattab, the Clear Quran
Notes placeholders
Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu

Ayatul Kursi

Yaseen

Al Mulk

Ar-Rahman

Al Waqi'ah

Al Kahf

Al Muzzammil

Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa