Ingia
🚀 Jiunge na Changamoto yetu ya Ramadhani!
Jifunze zaidi
🚀 Jiunge na Changamoto yetu ya Ramadhani!
Jifunze zaidi
Ingia
Ingia
Taarifa ya Sura
025

Sura Al-Furqan

Aya:

77

Mahali iliteremshwa:

Makka

Ali Muhsin Al-Barwani - Swahili Translation of Al-Muntakhab

SURAT AL FURQAN 

(Imeteremka Makka)

Idadi ya Aya za Sura hii ni 77. Zote ni za Makka isipo kuwa Aya 68, 69 na 70. Sura imeanzia kwa kubainisha cheo cha Qur'ani, na ukubwa wa ufalme wa Mwenye kuiteremsha ambaye ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Na juu ya utukufu wa utawala wake, washirikina bado badala yake wanaabudu masanamu, na wanaikadhibisha Qur'ani, na wanaukataa Utume wa Mtume s.a.w kwa hoja ya kuwa ati yeye ni binaadamu, anakula chakula, na anatembea masokoni, na kwa ubishi wanataka Malaika ndio wawaletee Ujumbe. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu amewafanya Mitume wake Malaika angeli wafanya ni watu ili wapate kufahamiana na watu. Ubabaishi unge baki. Na wakapinga kwa nini Qur'ani ikawa inateremka vipande vipande. Wakajibiwa hikima ya hayo. Na inda hii ikafuatilizwa kwa mifano yenye kueleza khabari za Mitume waliyo pita na kaumu zao. Lakini hizo kaumu zikafuata matamanio yao. Wakawa kama wanyama au wapotovu zaidi katika mwendo wao. Na zikaja Aya za uumbaji zenye kuonyesha ukamilifu wa kudra yake Mtukufu, yenye kufahamisha uangalizi na maarifa. Na Sura ikakhitimisha kwa kutaja sifa za Waumini zitazo warithisha vyumba vya Peponi vya juu, watakapo pokewa kwa maamkio na kusalimiwa.

He has revealed to you ËąO ProphetËş the Book in truth, confirming what came before it, as He revealed the Torah and the Gospel
— Dr. Mustafa Khattab, the Clear Quran
Notes placeholders
Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu

Ayatul Kursi

Yaseen

Al Mulk

Ar-Rahman

Al Waqi'ah

Al Kahf

Al Muzzammil

Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa