Aya:
40
Mahali iliteremshwa:
Makka
Ali Muhsin Al-Barwani - Swahili Translation of Al-Muntakhab
SURAT ANNABAA
(Imeteremka Makka)
Sura hi imethibitisha khabari ya kufufuliwa, na inawahadharisha hao wenye kutilia shaka jambo hilo. Na ikasimamisha hoja na dalili juu ya kuwezekana kwake kwa kuyaeleza yanayo onekana ya kudra ya Mwenyezi Mungu. Na ikatilia mkazo kuwepo kwake, na ikataja baadhi ya alama zake Kisha ikataja khatima ya wenye kuasi, nakhatima ya wachamngu. Na ikamalizikia kwa kuonya na kukhofisha kwa siku hiyo Inayo tisha.