🎯 Endelea kufuatilia!
Unda Lengo Langu
🎯 Endelea kufuatilia!
Unda Lengo Langu
Ingia
Ingia
Taarifa ya Sura
015

Sura Al-Hijr

Aya:

99

Mahali iliteremshwa:

Makka

SURATUL HIJR 

(Imeteremka Makka)

Suratul-Hijr ni Sura ya Makka. Nayo ina Aya 99. Imeanza kwa harufi za kutamkwa zenye kueleza kwamba Qur'ani imejengeka kwa harufi hizi hizi mnazo zitumia katike maneno yenu, na juu ya hivyo ni Muujiza kwenu, hamwezi kuleta kama hii. Kwani aliye iteremsha ni Mwenyezi Mungu, Aliye takasaika, na Akatukuka. Na hizo harufi pia ni kama kuwazindua wale wanao ipuuza Qur'anii, inawalingania, inawaita, waisikilize. Asaa wakanufaika, na wakahidika kumfuata Mwenyezi Mungu. 

Sura hii tukufu inabainisha ili watu wazingatie yaliyo wapata kaumu zilizo tangulia, na  khabari za Manabii walio kwisha pita, na yaliyo wapata kutokana na watu wao. Na pia Sura hii inaonyesha ishara za Mwenyezi Mungu katika ulimwengu, katika mbingu zilizo nyanyuliwa na zenye sayari ziilizo hifadhiwa, na ardhi iliyo tandikwa, na kukunjuliwa, na milima iliyo simama imara, na pepo zenye kubeba maji, na zenye kupandishia miti. 

Na Sura hii pia inaashiria mpambano wa mwanzo katika maumbile ya asli baina ya maluuni Iblisi na Adam na mkewe, na kuendelea mpambano huo baina ya kheri na shari mpaka imalizike dunia. Kisha tena malipo ya shari Siku ya Kiyama, na malipo ya kheri. Na baada ya hayo Mwenyezi Mungu anasimulia visa vya Manabii wawili, Ibrahim na Luutii, na watu wa Al Hijr. Na Sura inaeleza cheo cha Qur'ani, na hali ya washirikina katika kuipokea, na impasavyo Nabii kwa mnasaba wa ukafiri wao, navyo ni kufikisha ujumbe wake, na kuutangaza, na kumuabudu Mwenyezi Mungu mpaka ifike amri ya yakini.

He has revealed to you ˹O Prophet˺ the Book in truth, confirming what came before it, as He revealed the Torah and the Gospel
— Dr. Mustafa Khattab, the Clear Quran
Notes placeholders
Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu

Ayatul Kursi

Yaseen

Al Mulk

Ar-Rahman

Al Waqi'ah

Al Kahf

Al Muzzammil

Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa