🎯 Endelea kufuatilia!
Unda Lengo Langu
🎯 Endelea kufuatilia!
Unda Lengo Langu
Ingia
Ingia
Taarifa ya Sura
006

Sura Al-An-Am

Aya:

165

Mahali iliteremshwa:

Makka

SURAT AL - AN-A'AM 

(Imeteremka Makka)

SURA hii ni ya Makka isipo kuwa Aya hizi: 20, 23, 91, 93, 114, 141, 151, 152, na 153. Na Aya zake ni 165. Iliteremka baada ya Sura Al-Hijr. Na Sura hii tukufu imekusanya maana zilizo wekwa mbali mbali kama ifuatavyo:

  1. Imewazindua watu wauzingatie ulimwengu na dalili ziliomo ndani yake zenye kuonyesha Ubora wa aliye uumba, na Utukufu wake na Umoja wake wa pekee. na kuwa Yeye hashirikiani na yeyote, la katika kuumba, wala katika kuabudiwa wala katika dhati yake.
  2. Na imekusanya visa vya baadhi ya Manabii, na ikaanza kwa kisa cha Ibrahim (AS) kwa kubainisha kuwa alichukua maana ya ibada na Tawhidi kwa kuuchungua ulimwengu, na kufuata yaliyomo ndani yake. Naye alianza kwa kupeleleza nyota kisha mwezi, kisha jua, na akamalizia kwa kufuata ibada ya Mwenyezi Mungu pekee yake.
  3. Na ikapelekea macho yaangalie ajabu za uumbaji na vipi mambo yanavyo kuwa. Ikabainisha vipi kilicho hai kinyevu kinatokana na kisicho kuwa na uhai kikavu: na vipi mbegu inavyo pasuka na ukachipua mmea. 
  4. Na Sura hii imezitaja sifa za wapinzani, na vipi wanavyo shikilia ndoto zao zinazo watenga na Haki, na zinazo wapotosha. 
  5. Na ndani ya Sura hii umebainishwa uhalali wa vyakula alivyo halalisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na upotovu wa Washirikina walivyo jiharimishia wenyewe bila ya kutegemea dalili yoyote, na vipi wanavyo mnasibishia kuharimisha huko Mwenyezi Mungu Aliye Takasika. 
  6. Na ndani yake yamebainishwa mambo haya, ambayo ndio mukhtasari wa Uislamu na tabia njema za kusifika. Mambo yenyewe ni:- kuharimisha ushirikina, uzinzi, kuuwa mtu, kula mali ya yatima, waajibu wa kutimiza vipimo na mizani, kutimiza uadilifu, kutekeleza ahadi. kuwatendea wema wazazı, na kukataza kuwazika watoto wa kike nao wa hai.
He has revealed to you ˹O Prophet˺ the Book in truth, confirming what came before it, as He revealed the Torah and the Gospel
— Dr. Mustafa Khattab, the Clear Quran
Notes placeholders
Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu

Ayatul Kursi

Yaseen

Al Mulk

Ar-Rahman

Al Waqi'ah

Al Kahf

Al Muzzammil

Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa