Ingia
🚀 Jiunge na Changamoto yetu ya Ramadhani!
Jifunze zaidi
🚀 Jiunge na Changamoto yetu ya Ramadhani!
Jifunze zaidi
Ingia
Ingia
Taarifa ya Sura
022

Sura Al-Hajj

Aya:

78

Mahali iliteremshwa:

Madina

Ali Muhsin Al-Barwani - Swahili Translation of Al-Muntakhab

SURATUL HAJJ 

(Imeteremka Madina)

Sura hii ni ya Madina ila Aya 52, 53, 54, na 55. Aya zake ni sabiini na nane. Imeanzia kwa kuwaonya watu wamkhofu Mwenyezi Mungu, na kukumbusha vitisho vya Kiyama, na kuwajuilisha wanao bisha kwa upotovu na ujinga, na hayo yakafuatia kuletwa dalili za kufufuliwa, kwa kuleta sura ya mabadiliko katika kuumbwa binaadamu na kukua kwa mimea, na ikaeleza upinzani kumpinga Mwenyezi Mungu na matokeo yake. Na ikataja khabari ya Hija na kutukuza ibada zake. 

Na baada ya hayo Mwenyezi Mungu akaruhusu kupigana vita ya kujitetea. Na akafuatilizia hayo kumpoza Mtume s.a.w. kwa masaibu yaliyo kuwa yanampata kwa watu wake, kwa kutaja dhiki na mateso yaliyo wapata Mitume wa kabla yake. Na Aya za Sura hii zikabainisha dalili za uweza wake Mwenyezi Mungu Mtukufu na upweke wake, na mipaka ya kazi ya Mitume. Na kwamba hili ni onyo lisilo kimbilika. Na katika mwisho wa Sura wakasema hao wanao ambiwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu kwa kuzizuga akili za washirikina, kwamba hawawezi hata kuumba kiumbe kinyonge kabisa, naye ni nzi. Na nzi akiwapokonya kitu hawawezi kukipata kwake. 

Na Sura ikahimiza Sala, na Zaka, na Ibada, na Jihadi, bila ya kukusudia maovu. Kwani hii ni Dini ya baba yenu Ibrahim aliye mzaa Ismail, ambaye kutokana naye ndio wakazalika ukoo wa A'dnan. Na matokeo ya mambo yenu ni kuwa Mtume wenu akushuhudieni kwa kukufikishieni Ujumbe, na nyinyi mtoe ushahidi juu ya watu walio kwisha tangulia kwamba Mitume wao waliwafikishia Ujumbe kama ilivyo kujieni katika Qur'ani. Na Sura ikakhitimisha kwa kutaka kushikamana na Mwenyezi Mungu. Kwani Yeye ndiye bora ya Mlinzi, na bora ya Mwenye kunusuru.

He has revealed to you ËąO ProphetËş the Book in truth, confirming what came before it, as He revealed the Torah and the Gospel
— Dr. Mustafa Khattab, the Clear Quran
Notes placeholders
Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu

Ayatul Kursi

Yaseen

Al Mulk

Ar-Rahman

Al Waqi'ah

Al Kahf

Al Muzzammil

Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa