Aya:
6
Mahali iliteremshwa:
Makka
SURAT ANNAS
(Imeteremka Makka)
Katika Sura hii Mwenyezi Mungu anamuamrisha Nabii wake s.a.w. amwendee Yeye amwombe ulinzi kumkinga na shari kubwa zinazo washinda watu wengi kuzitambua kwa sababu zinatokana na matamanio yao, na pumbao lao, basi wakatumbukia katika yale yale wanayo katazwa.
Hiyo ndiyo shari ya wasiwasi wa Shetani, anaye jificha machoni, au hujidhihirisha kwe kificho; wasiwasi wake ni kwa hila na khadaa.