Aya:
52
Mahali iliteremshwa:
Makka
Ali Muhsin Al-Barwani - Swahili Translation of Al-Muntakhab
SURAT AL-QALAM
(Imeteremka Makka)
Sura hii tukufu imekusanya kumtetea Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w. na kuipelekea hima yake na azma yake hata abakie mwenye kushikilia Haki bila ya kumlegezea yeyote, na kushabihisha adhabu iliyo wapata watu wa Makka na adhabu iliyo wapata watu wenye shamba ambao kisa chao kimesimuliwa katika Sura. Na Waumini wanabashiriwa watayo yapata kutoka kwa Mola wao Mlezi: na hapana usawa baina yao na makafiri. Wanao kadhibisha wanakanywa madai yao wanao jidaia nafsi zao bila ya haki, na wanatiwa khofu kwa kuelezwa hali yao itakavyo kuwa Akhera, na wanatishwa. Na Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w. ananasihiwa asubiri na astahamili. Mwishoe Sura inakhitimisha kwa kuitukuza Qur'ani tukufu.