🎯 Endelea kufuatilia!
Unda Lengo Langu
🎯 Endelea kufuatilia!
Unda Lengo Langu
Ingia
Ingia
Taarifa ya Sura
061

Sura As-Saff

Aya:

14

Mahali iliteremshwa:

Madina

SURAT ASS'AF 

(Imeteremka Madina)

Sura hii imefunguka kwa kutoa khabari kwamba viliomo katika mbingu na katika ardhi vinamsabihi Mwenyezi Mungu. Na kwamba haiwaelekei Waumini kusema wasiyo yatenda. Na hakika Mwenyezi Mungu anapenda wawe mkono mmoja.

 Kisha Sura imewashutumu Wana wa Israili kuwa ni wenye inda na ukafiri kwa kauli za Mitume wawili watukufu, nao ni Musa na Isa s.a.w. Na kwamba wao wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuitimiza nuru yake. Na ndani ya hii Sura ipo ahadi ya Mwenyezi Mungu - na ahadi yake ni ya kweli - kuwa ataifanya Dini hii ishinde dini zote nyenginezo, hata walau washirikina wakichukia. Na ikakhitimishia kwa kuhimiza Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa hali na mali na kuwaahidi wenye kupigana Jihadi, Mujahidina, kupata msamaha na Pepo, na mengineyo wayapendayo Waumini, nayo ni msaada utokao kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi wa karibu. Na wanahimizwa Waumini wawe wenye kumsaidia Mwenyezi Mungu, kama walivyo kuwa wanafunzi wa Isa bin Mariamu. Na kwamba Mwenyezi Mungu atawaunga mkono waumini kwa msaada wake, na Yeye ni Mwenye kushinda  katika kila kitu, Mwenye hikima ya ukomo.

He has revealed to you ˹O Prophet˺ the Book in truth, confirming what came before it, as He revealed the Torah and the Gospel
— Dr. Mustafa Khattab, the Clear Quran
Notes placeholders
Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu

Ayatul Kursi

Yaseen

Al Mulk

Ar-Rahman

Al Waqi'ah

Al Kahf

Al Muzzammil

Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa