Aya
8
Mahali iliteremshwa
Makka
SURAT AT-TIN
(Imeteremka Makka)
Mwenyezi Mungu anaapa katika Sura hii kwa matunda mawili yenye baraka, na pahala pawili pazuri, ya kwamba Yeye hakika amemuumba mtu kwa njia kunjufu kabisa, kwa kumkamilishia akili, na uwezo wa kutaka na kutotaka, na mengineyo katika sifa za ukamilifu. Kisha Aya zikataja kuwa mtu hakusimama kwa mujibu wa alivyo umbiwa bali akateremka kwa daraja mpaka akawa wa chini kabisa, isipo kuwa walio amini na wakatenda mema kati yao. Hao Mwenyezi Mungu amewakunjulia vipawa. Kisha Sura imewageukia kuwakemea wanao kadhibisha kufufuliwa baada ya kudhihiri dalili zote za uweza wa Mwenyezi Mungu na khabari za hikima yake.