Ingia
🎯 Endelea kufuatilia!
Unda Lengo Langu
🎯 Endelea kufuatilia!
Unda Lengo Langu
Ingia
Ingia
Taarifa ya Sura
029

Sura Al-Ankabuut

Aya:

69

Mahali iliteremshwa:

Makka

SURAT AL A'NKABUT 

(Imeteremka Makka)

SURA HII NI ya Makka, na idadi ya Aya zake ni 69. Lakini Aya 1 mpaka 11 ziliteremka Madina. Sura hii imeanzia kwa kubainisha kwamba hapana budi ila Imani ya Waumini itiwe mitihanini kwa misukosuko na jihadi kwa ajili ya kulinda dola ya Haki na Imani. Na binaadamu ameusiwa kwa wazazi wake pamoja na amri ya jihadi, il ukusanyike wema na jihadi, na baina ya watu wa namna mbali mbali na Imani. Na imeelezwa kwamba miongoni mwao yupo anaye sema kwa ulimi wake kwamba ameamini na hali moyo wake haukukubali. 

Kisha Sura hii imetaja khabari za Nuhu na kaumu yake, na kadhaalika imeeleza kisa cha Ibrahim katika wito wake. Na ikabainisha mafunzo hayo kwa ajili ya Mtume s.a.w. Kisha ikasimulia jawabu ya watu wa Ibrahim Na ikaeleza khabari za Luti na kisa cha kaumu yake, na kuteremka kwa Wajumbe Malaika wa Mwenyezi Mungu kuja kuwahiliki, na wakaokoka ahali zake isipo kuwa mkewe. Kisha Subhanahu akaashiria kisa cha Shuaibu pamoja na Madyana, na cha Hud na A'di, na Saleh na Thamud, na kudanganyikiwa kwa Qaruni na Firauni na Hamani na matokeo ya mwisho wao.

 Na Yeye Subhanahu amebainisha kwamba kuabudu masanamu kwa washirikina kunategemea hoja iliyo kuwa dhaifu kabisa kuliko jumba la buibui. Na kwamba mifano kama hii hawaielewi ila wale wanao tumia akili zao. Na baada ya hayo Mwenyezi Mungu akamuamrisha Nabii wake asijadiliane na Watu Wa Kitabu ila kwa njia nzuri. Na Yeye Subhanahu akaashiria kwamba Nabii s.a.w. hajui kusoma wala kuandika, na hayo yanazidi kuonyesha Utume wake. 

Na pia Subhanahu ametaja ukaidi wa washirikina katika kutaka kwao waletewe miujiza ya kuiona, nayo wataikataa kama walivyo ikataa kaumu ya Musa  na wengineo. Na akagusia kule kuhimiza kwao kuteremshiwa adhabu. Naye amewabainishia adhabu itakayo wapata. Naye Subhanahu akataja malipo ya Waumini na Makafiri Siku ya Kiyama,  na akataka watu watazame baada ya hayo ulimwengu na neema Za Mwenyezi Mungu Mtukufu ziliomo ndani yake. 

Kisha akataja thamani ya uhai wa duniani ukilinganisha na wa Akhera, na hali ya washirikina katika unyonge wao na kumkimbilia kwao Mwenyezi Mungu wanapo kuwa katika khofu, na wanapo kuwa na nguvu na wakawa katika usalama wanavyo mshirikisha Mwenyezi Mungu. Kisha akaeleza neema zake anazo wapa katika Nyumba Takatifu ya Makka, na wanavyo zikanya neema hizo. Kisha Mwenyezi Mungu akabainisha fadhila za wanao pigana Jihadi.

He has revealed to you ˹O Prophet˺ the Book in truth, confirming what came before it, as He revealed the Torah and the Gospel
— Dr. Mustafa Khattab, the Clear Quran
Notes placeholders
Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu

Ayatul Kursi

Yaseen

Al Mulk

Ar-Rahman

Al Waqi'ah

Al Kahf

Al Muzzammil

Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa