Aya
64
Mahali iliteremshwa
Madina
SURATUN NUR
(Imeteremka Madina)
Sura hii ni ya Madina, na Aya zake ni 64. Mwenyezi Mungu amebainisha ndani yake waajibu wa kusafisha umma na uchafu wa zina na kutangaza fedheha kwa vitendo na maneno kati ya Waumini. Na akaleta sharia ya adhabu kuzuia hayo, kama alivyo leta sharia makhsusi katika uzinzi wa mume au mke ili kujenga imani baina ya mtu na mkewe. Kutoka uzinzi masimulizi yakaingilia kutaja hukumu ya uwongo katika hali hizi, na yawapasayo Waumini kwa mintarafu ya neno ovu lisio kuwa na dalili.
Tena yakafuatia masimulizi ya adabu za kuingia majumbani. Na nani mwenye haki ya kuona pambo la mwanamke. Na baada ya wito wa jumla ikafuatiliza kutakiwa mwendo safi usio na towa. Kisha imekuja Nuru ya Mwenyezi Mungu, na inatajwa misikiti, na vinatangazwa vitendo vya makafiri na hali za wenye inadi. Na upande mwengine zinaelezwa hali za Waumini. Baada ya hayo Sura inaeleza adabu za watu wa nyumbani, watu walio khusiana, watoto na wakubwa, katika hali ya kuingiliana na kuchanganyika. Na nani mwenye haki ye kula naye mtu. Na khatimaye zimetajwa sifa za Waumini wanapo itwa na Mtume kwa jambo lilio wakhusu wote, na Sura ikambainisha Mwenye Ukuu wa Ufalme wake ulio tukuka, na Mwenye kuenea ujuzi wake.