🎯 Endelea kufuatilia!
Unda Lengo Langu
🎯 Endelea kufuatilia!
Unda Lengo Langu
Ingia
Ingia
Taarifa ya Sura
027

Sura An-Naml

Aya:

93

Mahali iliteremshwa:

Makka

SURAT AN-NAML 

(Imeteremka Makka)

SURA AN-NAML ni ya Makka. Aya zake ni 93. Imeanza kwa harufi za kutamkwa, kukumbusha cheo cha Qur'ani ambayo imetoka katika jinsi ya maneno ya Kiarabu. Na juu ya hivyo imewashinda hao Waarabu kuleta mfano wake. Na tena pia ni kama kumzindua aliye ghafilika aisikilize. Baada yake kimekuja kisa cha Musa (AS) Na imetajwa baadhi ya miujiza yake, na kisa cha Daudi (AS) na kurithiwa kwake na mwanawe, Mfalme Sulaiman, na kukusanyika majini, na watu, na ndege kwa ajili yake. Na imetajwa kufahamu kwake Sulaiman maneno ya wanyama, na shukrani yake kwa neema hii. Kisha kutoweka ndege Hud-hud, na akaja na kisa cha Balqis, na kuabudu kwake bibi huyu na watu wake kuliabudu jua. Tena Sulaiman akampelekea barua, naye akamjibu kwa kumpelekea zawadi baada ya kushauriana na watu wake, na ikaelezwa kuletwa kiti chake cha enzi kwa njia ya mwenye ilimu ya Kitabu, na kuingia kwake huyo bibi katika qasri (jumba la kifalme) la Sulaiman, nalo likamshitua, na akatangaza ut'iifu wake na Imani yake kumuamini Sulaiman. 

Na Sura hii imetaja hadithi ya Saleh (AS) na kaumu yake, na hadithi ya Luti (AS) na kaumu yake, na kuvuka kwake, na kuangamia kwa mafisadi. Na Sura tukufu hii imezindua ziangaliwe dalili za aliye umba mbingu na ardhi zenye kuthibitisha uwezo wake na upweke wake.

Na ikaashiria cheo cha Qur'anii tukufu katika kazi ya Daa'wa (Wito), na vipi washirikina wanavyo ipuuza juu ya kuwa muujiza wake umekamilika. Na imetaja yatakayo kuwa atakapo toka mnyama akisema na watu kuwa walikuwa hawana yakini ya Ishara Zetu. Kisha Sura ikaelekea ulimwengu, na vipi watakavyo fazaika waliomo wakati wa mpulizo wa kufufuliwa na kukusanywa. Na ikanabihisha hali ya ardhi, na kwamba milima yake inakwenda kama yaendavyo mawingu, na ikasimulia yanayo mfuatia Mtume takasika katika kazi yake ya Daa'wa, na kwamba ni waajibu Mwenyezi Mungu Alilye takasika asifiwe.

He has revealed to you ˹O Prophet˺ the Book in truth, confirming what came before it, as He revealed the Torah and the Gospel
— Dr. Mustafa Khattab, the Clear Quran
Notes placeholders
Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu

Ayatul Kursi

Yaseen

Al Mulk

Ar-Rahman

Al Waqi'ah

Al Kahf

Al Muzzammil

Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa