Makka
Sura Al-Qiyama

Aya

40

Mahali iliteremshwa

Makka

SURAT AL-QIYAMAH 

(Imeteremka Makka)

Sura hii tukufu inasimulia khabari za kufufuliwa watu na kuhisabiwa, na khabari za Kiyama na vitisho yake. Kisha inampa moyo Mtume s.a.w. kuwa Qur’ani itakusanywa yote katika kifua chake, na Sura ikageuka kuwakemea hao wanao penda yapitayo njia ya duniani, wakaacha ya Akhera, na ikalinganisha baina ya nyuso za Waumini zenye kung'aa na nyuso za makafiri zilizo kunjana. Na imezungumzia pia hali ya mtu aliye mguu mmoja uko kaburini, na aliyo nayo ya upungufu katika yaliyo kuwa yakimlazimu, hata akawa kama kwamba anadhani kuwa hatahisabiwa yeye. Na mwishoe Sura imekhitimisha kwa dalili zinazo pelekea lazima tuamini kuwa kufufuliwa kupo.