Makka
Sura Al-Muuminun

Aya

118

Mahali iliteremshwa

Makka

SURATUL MUUMINUN 

(Imeteremka Makka)

HII NI SURA iliyo teremka Makka. Aya zake ni mia na kumi na nane. Imeanza kwa kuthibitisha mafanikio ya Waumini, na ikafuatia kueleza sifa zao. Kisha ikataja asli ya kuumbwa mwanaadamu, na kubadilika kwake kwa kukua, na kuzalikana vizazi vyake, na baadhi ya mambo yanayo dhihirisha uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. 

Tena zikafuatia hadithi za Manabii zinazo fanana kwa umoja Wa ujumbe na umoja Wa binaadamu, ijapo kuwa watu wange khitalifiana baina ya wanao kubali na wanao kengeuka. Na sura hii imeeleza khabari za mwenye kutaka uwongofu, na mwenye kupotoka, na msimamo wa washirikina mbele ya Nabii s.a.w. Tena ikaingia kueleza yanayo onekana ya uwezo wa Mwenyezi Mungu katika hukumu za kumuumba mwanaadamu. 

Na Mwenyezi Mungu Subhanahu kaingia kuwauliza watu wamjibu kwa kutumia akili zao za maumbile kwa yanayo thibitisha kuwepo kwake, na kuthibitisha Ungu wake. Kisha Sura hii ikaeleza hali za watu itakavyo kuwa Siku ya Kiyama, na kwamba wao watahisabiwa, na watafanyiwa uadilifu. Tena Sura inakhitimisha kubainisha Utukufu wake Subhanahu wa Taa'la, na kumnabihisha Nabii wake aombe maghfira na rehema kutokana na Mbora wa wenye kurehemu.