Aya
3
Mahali iliteremshwa
Makka
SURAT ALKAWTHAR
(Imeteremka Makka)
Mwenyezi Mungu katika Sura hii anamtajia Mtume wake s.a.w. neema alizo mfanyia kwa kumpa kheri nyingi na neema kubwa kubwa katika dunia na Akhera, na akamtaka adumishe Sala iliyo safi kwa kumridhi Mwenyezi Mungu, na atoe mhanga bora ya mali yake kwa dhahiya ya shukrani kwa ukarimu alio pewa. Kisha Sura imekhitimisha kwa kumbashiria Nabii s.a.w. kuwa atakatiliwa mbali huyo anaye mchukia na kumbughudhi Mtume.