Ingia
🚀 Jiunge na Changamoto yetu ya Ramadhani!
Jifunze zaidi
🚀 Jiunge na Changamoto yetu ya Ramadhani!
Jifunze zaidi
Ingia
Ingia
Taarifa ya Sura
018

Sura Al-Kahf

Aya:

110

Mahali iliteremshwa:

Makka

Ali Muhsin Al-Barwani - Swahili Translation of Al-Muntakhab

SURA AL KAHF 

(Imeteremka Makka)

Sura hii ni ya Makka, isipo kuwa Aya 38, na Aya zinazo anzia 83 mpaka 101. Basi zimo Aya ishirini za Madina. Nayo imeanzia kwa kumhimidi Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuiteremsha Qur'ani Tukufu, na kubainisha kuwa Qur'ani ni onyo na bishara. Ndani yake lipo onyo kwa wanao dai kuwa ati Mwenyezi Mungu ana mwana. Na humu imetajwa hamu kubwa aliyo nayo Nabii ya kutaka waamini wale anao waita kwenye mlingano wa Mwenyezi Mungu. Kisha kikatajwa kisa cha Ahlil Kahf, Watu wa Pangoni, walio lala usingizi kisha wakaamka baada ya kukaa katika pango lao muda wa miaka mia tatu na tena wakazidishiwa tisa. Na watu hao walikuwa Wakristo walio kuwa wakikimbia udhalimu wa mtawala wa Kirumi. Wakalala katika pango muda huo, kisha wakaamka ili kuwa ni ishara ya uweza wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kufufua baada ya kufa.

Kisha baada ya hayo Mwenyezi Mungu akamuamrisha kusoma Qur'ani na aitumie kwa kuonya na kubashiri. Kisha imebainishwa hali ya watu wa Peponi na watu wa Motoni. Na Mwenyezi Mungu akapiga mifano ya watu wawili, mmoja tajiri anajitapa kwa mali yake na wanawe. Na wa pili anatafakhari kwa Mwenyezi Mungu wake. Na amebainisha Subhanahu kuwa ulinzi wake ndio wa Haki. Na tena Subhanahu ameeleza starehe ya duniani inayo pita, na neema ya daima au adhabu chungu ya Siku ya Kiyama. Tena Subhanahu ametaja hadithi ya Musa pamoja na Mja Mwema aliye pewa ilimu kutokana na Mwenyezi Mungu. Na katika kisa hichi inapatikana sura ya vipi mtu anaweza asijue mambo, hata akiwa Nabii Mtume katika Mitume imara - Ulul a'zmi - kwa kudra yake Mwenyezi Mungu, ila akiwa Yeye Mwenyezi Mungu akimjuulisha. Tena anatajwa Dhul-qarnaini na kufika kwake mashariki ya mbali, na alivyo jenga Ukuta. Kisha yatakayo kuwa Siku ya Kiyama, na malipo ya Waumini, na ilimu ya Mwenyezi Mungu na maneno yake yasiyo malizika. Na Sura ikakhitimisha kwa kueleza Njia ya Kumridhi Subhanahu.

He has revealed to you ËąO ProphetËş the Book in truth, confirming what came before it, as He revealed the Torah and the Gospel
— Dr. Mustafa Khattab, the Clear Quran
Notes placeholders
Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu

Ayatul Kursi

Yaseen

Al Mulk

Ar-Rahman

Al Waqi'ah

Al Kahf

Al Muzzammil

Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa