Aya
28
Mahali iliteremshwa
Makka
SURAT AL-JINN
(Imeteremka Makka)
Mwenyezi Mungu Mtukufu amemuamrisha Mtume wake s.a.w. katika Sura hii tukufu awafikishie watu aliyo funuliwa yeye kwa wahyi, kwamba majini wameisikiliza Qur'ani na wameitikia wito wake, na kuwapa khabari kwa yaliyo wapata wapumbavu wao na wema wao, na yaliyo kuwa kutokana na kukaa kwao kusikiliza kwa wizi, na kufukuzwa kwao hivi sasa. Na Aya za Sura hii zinaeleza khabari za hao wanao nyatia kwenye njia ya Uislamu na kuupinga, na ikasimulia juu ya kuisafishia misikiti kwa ajili ya kumuabudu Mwenyezi Mungu tu peke yake, na juu ya wito wa Mtume kumwendea Mwenyezi Mungu, na majini kumzunguka Mtume, na ikaeleza kwa kuwekea mipaka lipi aliwezalo Mtume na lipi ambalo haliwezi, na ikahadhirisha wenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume watahadhari na Jahannamu na kubakia humo milele.
Na mwishoe Sura ikakhitimisha kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliye khusika na kuijua ilimu ya ghaibu, mambo yasiyo onekana, na humdokezea anaye mteuwa katika viumbe ili awe ni Mtume wa kuuhifadhi Wahyi kwa kuulinda mpaka awafikishie watu kwa utimilivu. Na Mwenyezi Mungu anayajua hayo.