Madina
Sura Ad-Dahr

Aya

31

Mahali iliteremshwa

Madina

SURAT AL-INSAN 

(Imeteremka Madina)

Sura hii imekusanya maneno juu ya kuumbwa kwa binaadamu na kujaribiwa kwake, na kutayarishwa kwake aweze kumshukuru Mwenyezi Mungu au kumkufuru. Na imekusanya mazungumzo juu ya malipo ya makafiri; na imefafanua neema alizo wafadhili Mwenyezi Mungu Waumini, kisha ikageukia kusema na Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w. na kumtajia alivyo neemeshwa kwa kuteremshiwa Qur’ani, na ikamuamrisha asubiri na adumu katika utiifu. Na Sura inawaonya wanao ipenda dunia na wakaifadhilisha Kuliko Akhera, na ikasimulia kwa mawaidha ya Aya hizi, na ikakhusisha kunafiika kwazo pindi akipenda Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ikazifanya rehema za Mwenyezi Mungu na adhabu zake kuwa zinategemea hukumu yake na pendo lake.