Aya
26
Mahali iliteremshwa
Makka
SURAT AL-GHAASHIYAH
(Imeteremka Makka)
Imeanza Sura hii kwa njia ya kutia shauku kuisikiliza hadithi ya Siku ya Kiyama, na hayo mambo yatakayo tokea humo. Inaashiria kwamba watu ni makundi mawili miongoni mwao wapo ambao hawatapata hishima yoyote kwa watakavyo pokewa na wataingia kwenye Moto mkali. Na wapo watakao ifikia siku hiyo kwa furaha kwa namna ya rehema na radhi zilizo andaliwa kwa ajili yao. Kisha Sura ikaeleza dalili zilizo wazi za uweza wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kufufua kutokana na wanavyo ona wenyewe kwa macho yao na wanayo nafika kwayo katika uhai wao. Na baada ya kuzitaja dalili hizi ikageukia khabari za Mtume s.a.w. kwa kukumbusha kwamba waajibu wake mkubwa kwa mintarafu yao ni wazi, ya kwamba yeye hakutawalishwa juu yao awalazimishe kuamini, na kwamba mwenye kugeuka na akakufuru baada ya waadhi huu ni Mwenyezi Mungu ndiye atakaye mshika kwa dhambi zake, na atamuadhibu kwa adhabu kubwa kabisa, atapo rejea kwake baada ya kufa, kwan marejeo ya wote na kuhisabiwa kwao wote ni kwake Yeye Mwenyezi Mungu.