Aya
5
Mahali iliteremshwa
Makka
SURAT AL-FIIL
(Imeteremka Makka)
Mwenyezi Mungu anampa khabari Mtume wake s.a.w. kisa cha Watu wa Tembo (Ndovu) walio kusudia kuivunja Nyumba ya Mwenyezi Mungu ya Al-Kaaba, na anakionyesha kisa hichi kuwa ni dalili ya uweza wake Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kujilipizia kwake juu ya hao wanao vunja vitu vyake vitakatifu. Mwenyezi Mungu hakika aliwasalitishia majeshi yalio wang'oa mizizi yao, na wasibakie kitu ila kama nazi iliyo liwa na mwezi.