Makka
Sura Al-Fatihah

Aya

7

Mahali iliteremshwa

Makka

SURAT AL-FAATIH’A

(Imeteremka Makka)

Sura hii iliteremka Makka kabla ya Hijra (kuhamia Mtume s.a.w. Madina). Imeitwa Al-Faatiha yaani Kifungulio kwa kuwa ndiyo sura ya mwanzo katika mpango wa Msahafu Mtukufu, nayo ni sura ya mwanzo iliyo teremka kwa utimilivu wake. Na sura hii inakusanya jumla ya yaliyomo katika Qur'ani na kama kwamba huu ni mukhtasari wake, na baadaye yatakuja mambo kwa tafsili, babu babu.

Na makusudio ya Qur'ani ni: Kubainisha Tawhid ambayo ni Upweke wa Mwenyezi Mungu; na kubainisha ahadi na bishara kwa Muumini mtenda mema: na kubainisha ahadi na onyo kwa kafiri na mtenda maovu; na kubainisha ibada; na kubainisha njia ya kufanikiwa duniani na Akhera; na hadithi za walio mtii Mwenyezi Mungu wakafuzu, na hadithi za walio muasi wakaangamia. 

Sura Al-Faatiha inakusanya kwa ufupi na kwa kuashiria makusudio haya, na kwa hivyo ndio ikaitwa pia "Ummul Kitaab" yaani 'Msingi wa Kitabu".