Makka
Sura Al-Falaq

Aya

5

Mahali iliteremshwa

Makka

SURAT AL-FALAQ 

(Imeteremka Makka)

Sura hii inamtaka Nabii s.a.w. amwendee Mola wake Mlezi atake ulinzi kwake kujilinda na shari ya kila mwenye shari, ya viumbe vyake, na shari za usiku linapo ingia giza, yanayo yasibu nafsi katika hali ya upweke, na madhara ambayo mtu hawezi kujikinga nayo, na shari za mafisadi wanao pita kuharibu makhusiano na mawasiliano yalio baina ya watu, na shari za hasidi anaye tamani kuondoa neema alizo wapa Mwenyezi Mungu waja wake.