Aya:
75
Mahali iliteremshwa:
Madina
Ali Muhsin Al-Barwani - Swahili Translation of Al-Muntakhab
SURAT AL ANFAAL
(Imeteremka Madina)
Surat Al Anfaal hii imeteremka Madina. Aya zake ni 75. Mwenyezi Mungu aliye takasika na kutukuka, amebainisha katika Sura hii baadhi ya hukumu za vita, na mambo yanayo pelekea vita, na sababu za ushindi, na makamo ya nguvu za moyo zinazo pelekea kushinda, na hukumu za ngawira za vita, na wakati gani kuchukua mateka.
Na Mwenyezi Mungu kwa hikima yake amekusanya humu hukumu za kisharia. Sura hii inaeleza kisa cha Vita vya Badri, na baadhi ya yaliyo kuwa kabla yake, na kuashiria sababu zilizo sabibisha hivyo vita, nazo ni kutoka makafiri washirikina Makka kumwendea Nabii s.a.w. Na humu Mwenyezi Mungu anataja ujitayarisha kwa vita, na kupasa kuelekea salama na amani ikiwa maadui wanaelekea kutaka salama.
Na Sura hii tukufu inamalizikia kubainisha urafiki wa Waumini, wao kwa wao; na kuwawajibikia Waumini kuihama nchi inayo waonea na kuwafanya wanyonge, ili wende kuwaunga mkono Waumini wenzao katika juhudi ya kutukuza Uislamu na Waislamu.
Michango ya kila mwezi hutusaidia kuboresha Quran.com na kuendeleza shughuli zetu, ili tuweke mkazo mdogo kwenye ukusanyaji wa fedha na zaidi kwenye kuleta athari chanya Jifunze zaidi