Aya
11
Mahali iliteremshwa
Makka
SURAT WADH-DHUH'AA
(Imeteremka Makka)
Sura hii imeanza kwa viapo viwili vyenye kueleza nyakati mbili za uchangamfu na za kutulia, ya kwamba kwa hakika Mwenyezi Mungu hakumwacha Mtume wake wala hakumchukia, na kwamba aliyo mtengenezea katika Akhera makao ya juu ni bora zaidi kuliko alio mkirimu duniani. Kisha Subhanahu akaapa kwamba Yeye atampa mpaka aridhike, na yaliyo tangulia ni ushahidi wa yatakayo kuja. Kwani alikuwa yatima akampatia makaazi; alikuwa amepotea akampa bora ya uwongofu, na alikuwa fakiri akamtajirisha. Kisha Aya zikataka aangaliwe vyema yatima, na asikemewe mwenye kuomba au kuuliza, na zisimuliwe neema za Mwenyezi Mungu.