Sema: Yule aliye katika upotovu, basi Arrahmani (Mwingi wa rehema) na amuongezee (muda, mali na mengineyo) mpaka atakapoona yale waliyoahidiwa - ima ni adhabu au ni Saa, hapo ndipo watakapojua ni nani mwenye makao maovu zaidi na mwenye jeshi dhaifu zaidi.