Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Hud 11:57 فان تولوا فقد ابلغتكم ما ارسلت به اليكم ويستخلف ربي قوما غيركم ولا تضرونه شييا ان ربي على كل شيء حفيظ ٥٧

Ukurasa 228 · Juzuu 12

فَإِن
تَوَلَّوۡاْ
فَقَدۡ
أَبۡلَغۡتُكُم
مَّآ
أُرۡسِلۡتُ
بِهِۦٓ
إِلَيۡكُمۡۚ
وَيَسۡتَخۡلِفُ
رَبِّي
قَوۡمًا
غَيۡرَكُمۡ
وَلَا
تَضُرُّونَهُۥ
شَيۡـًٔاۚ
إِنَّ
رَبِّي
عَلَىٰ
كُلِّ
شَيۡءٍ
حَفِيظٞ
٥٧
Na wakikengeuka, "Basi hakika mimi nimekwishawafikishia yale niliyotumwa nayo kwenu. Na Mola wangu Mlezi atawaleta watu wengine badala yenu, wala nyinyi hamumdhuru kitu Yeye. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kuhifadhi vyema kila kitu."
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Ibn Kathir (Abridged)

وَيَسْتَخْلِفُ رَبِّى قَوْمًا غَيْرَكُمْ

(My Lord will make another people succeed you, ) This refers to a group of people who will worship Allah alone, without associating anything with Him. This also implies that the polytheists do not bother Allah and they do not harm Him in the least with their d

…

وَيَسْتَخْلِفُ رَبِّى قَوْمًا غَيْرَكُمْ

(My Lord will make another people succeed you, ) This refers to a group of people who will worship Allah alone

…
Tazama Tafsir

Soma katika Muktadha

50. Na kwa kina 'Aadi tulimtuma ndugu yao Hud. Akasema, "Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu! Hamna mungu isipokuwa Yeye tu. Nyinyi si chochote isipokuwa ni wazushi tu. 51. Enyi watu wangu! Siwaombi ujira kwa ajili ya haya. Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Yule aliyeniumba. Basi hamtumii akili? 52. Na enyi kaumu yangu! Mwombeni msamaha Mola wenu Mlezi, kisha mtubie kwake. Atawatumia mbingu zenye kunyesha mvua ya kumiminika kwa wingi, na atawazidishia nguvu juu ya nguvu zenu. Wala msigeuke mkawa wahalifu." 53. Wakasema, "Ewe Hud! Hujatuletea ushahidi ulio wazi. Wala sisi hatuiachi miungu yetu kwa kufuata kauli yako. Na wala sisi hatukuamini wewe. 54. Sisi tunasema: ʻBaadhi ya miungu yetu imekusibu kwa baa.ʼˮ Akasema, “Hakika, mimi ninamshuhudisha Mwenyezi Mungu, na nyinyi shuhudieni, ya kwamba mimi niko mbali na hao mnaowafanya washirika. 55. Badala ya Yeye. Basi nyinyi nyote nipangieni njama, na kisha msinipe muhula! 56. Hakika mimi nimemtegemea Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Hakuna kiumbe yeyote isipokuwa Yeye anamwendesha atakavyo. Hakika Mola wangu Mlezi yuko kwenye njia iliyonyooka." 57. Na wakikengeuka, "Basi hakika mimi nimekwishawafikishia yale niliyotumwa nayo kwenu. Na Mola wangu Mlezi atawaleta watu wengine badala yenu, wala nyinyi hamumdhuru kitu Yeye. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kuhifadhi vyema kila kitu." 58. Na ilipofika amri yetu, tulimwokoa Hud na wale walioamini pamoja naye, kwa rehema itokayo kwetu. Na tukawaokoa kutokana na adhabu nzito. 59. Na hao ndio kina 'Aadi. Walizikufuru Ishara za Mola wao Mlezi, na wakawaasi Mitume wake, na wakafuata amri ya kila jabari mkaidi. 60. Na wakafuatishiwa laana katika dunia hii na Siku ya Kiyama. Basi tambueni mtanabahi kuwa hakika kina 'Aadi walimkufuru Mola wao Mlezi. Na tambueni mtanabahi kuwa hakika waliangamizwa kina 'Aadi, kaumu ya Hud.

- Swahili Translation - Rowad Translation Center

Endelea Kusoma

Maelezo na Tafakari

Huna maelezo au tafakari yoyote kuhusu aya hii.

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia