Soma na usikilize Sura Fatir pamoja na tarjuma yake, tafsir, usomaji wa sauti, maana ya neno kwa neno, na unukuzi pia. Tarjuma ya Ali Muhsin Al-Barwani.
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu
Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na ardhi, aliye wafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa, mbili-mbili, na tatu- tatu, na nne-nne. Huzidisha katika kuumba apendavyo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu. 1