Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko, (1) Na shari ya alivyo viumba, (2) Na shari ya giza la usiku liingiapo, (3) Na shari ya wanao pulizia mafundoni, (4) Na shari ya hasidi anapo husudu. (5)
–Sura Al-Falaq [113:1-5]
قل اعوذ برب الناس ١ ملك الناس ٢ الاه الناس ٣ من شر الوسواس الخناس ٤ الذي يوسوس في صدور الناس ٥ من الجنة والناس ٦
Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu, (1) Mfalme wa wanaadamu, (2) Mungu wa wanaadamu, (3) Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas, (4) Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu, (5) Kutokana na majini na wanaadamu. (6)